Kofi Annan

31 Desemba 2018

Jarida letu la kufunga mwaka hii leo ni mkusanyiko wa matukio  ya mwaka ukiletwa kwako na Siraj Kalyango na Grace Kaneiya. Hata hivyo kuna muhtasari wa habari muhimu hivi leo ikiwemo uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti -
9'55"

UN yamkumbuka Annan, amwagiwa sifa lukuki

Umoja wa Mataifa leo umekuwa na kumbukumbu maalum ya Katibu Mkuu wa 7 wa chombo hicho aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 80.

Katibu Mkuu wa UN asema Kofi Annan na UM havitenganishiki

Leo ni siku ya amani duniani ambapo Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku hiyo kwa matukio mawili ya kupiga kengele ya aman ina kufanya kumbukizi maalum ya Katibu Mkuu wake wa 7 Kofi Annan. 

Sauti -
1'45"

21 Septemba 2018

Kofi Annan aenziwa Umoja wa  Mataifa, Guterres asema hauwezi kumtenganisha Kofi na Umoja wa Mataifa. Tunabisha hodi Sudan Kusini vijana wazungumzia kuhusu amani ya nchi hiyo. Je wanataka nini?

Sauti -
12'1"

Kofi Annan kuenziwa na UN katika siku ya amani duniani hii leo

Umoja wa Mataifa leo utakuwa na tukio maalum la kumkumbuka Katibu wake mkuu wa 7 Kofi Annan aliyefariki dunia mwezi uliopita huko Uswisi na kuzikwa wiki iliyopita nyumbani kwake nchini Ghana.

Kofi alizungumza bila hata kutamka neno- Guterres

Tangu kifo cha Kofi Annan, nimekuwa nikitafakari ni kitu gani kilimfanya awe wa kipekee!

Sauti -
3'34"

13 Septemba 2018

Mwendazake Kofi Annan, azikwa leo huko Ghana, Katibu Mkuu Antonio Guterres afunguka. Keating ahitimisha jukumu lake Somalia apazia sauti vyombo vya kimataifa vya  habari.

Sauti -
11'14"

Sasa nimetambua upekee wa Annan- Guterres

Tangu kifo cha Kofi Annan, nimekuwa nikitafakari ni kitu gani kilimfanya awe wa kipekee! Hivi ndivyo ambavyo Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaeleza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mmoja wa watangulizi wake Kofi Annan aliyezikwa leo huko Accra nchini Ghana. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Annan kuzikwa leo Accra, Guterres kushiriki

Macho na masikio leo yanaelekezwa huko Accra Ghana kwenye mazishi ya mwanadiplomasia nguli na Katibu Mkuu wa 7 wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan aliyefariki dunia mwezi uliopita.

Kofi alikuwa nasi Kenya wakati wa shida- Balozi Macharia

Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi maalum ya Katibu Mkuu wa 7 wa chombo hicho, Kofi Annan aliyefariki dunia tarehe 18 mwezi huu wa Agosti huko Uswisi baada  ya kuugua kwa muda mfupi.

Sauti -
2'27"