UNHCR kusaidia wakimbizi wa ndani Libya kurejea nyumbani

15 Agosti 2018

Baada ya zaidi ya miaka 7 ukimbizini ndani ya nchi yao ,  hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeanza kuwawawezesha baadhi ya wakazi wa jimbo la Tawerga nchini Libya kurejea nyumbani.

Bi Amina na mwanae Suhaib ni miongoni mwa  zaidi ya wakimbizi wa ndani 40,000 kutoka mji wa Tawergha ambao walilazimika kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011 vilivyolipukakatika jimbo la Misrata na vitongiji vyake.

Toka hapo, ni  miaka 7  ambapo yeye na jamaa zake wanaishi katika  makazi ya kuhamahama ya yaliyopo nje kidogo ya mji mkuu Tripoli.

Sauti ya Amina

Tuliishi katika chumba kimoja kwa zaidi ya miaka 2. Nilipikia humo na kualala humo humo ,mpaka wahisani walipotusaidia.”

Wingi wa watu na ukosefu wa mahitaji muhimu umefanya makazi  hayo kukosa hadhi ya kuishi binadamu, hivyo kusababisha  UNHCR kuingilia kati ili kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo.

Sauti ya Amina

Ni Dhahiri nataka kurudi nyumbani  na kuishi Tawergha, ila tuwe salama bila wasiwasi. Sitaki kuona watoto wetu wakitekwa nyara. Na hatutaki kushambuliwa. Ningependa kwenda nyumbani katika hali ya  usalama.

Amina anatamani mwanae Suhaib akapaone nyumbani kwao kwa kuwa amezaliwa ukimbizini.

Zaidi ya walibya 180,000 wako ukimbizi katika nchi yao kufuatia migogoro ya kivita inayoendelea nchini humo tangu mwaka 2011 vilivyosababisha Muammar Al Gathafi kuondolewa madarakani.

UNHCR na washirika wake wamekuwa mstari wa mbele kuwawezesha maelfu ya wakimbizi kurejea nyumbani.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter