Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL amesema anasikitika kwamba makubaliano ya Berlin ya usitishaji uhasama nchini Libya yanatekelezwa kwa jina tu na si kwa vitendo.
Watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na shambulizi la anga lililolenga Chuo cha kijeshi huko Hadaba, kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linahofia usalama wa mamia ya wakimbizi na waomba hifadhi waliokusanyika katika kituo cha makutano na kuondoka (GDF) kilichopo mjini Tripoli nchini Libya.
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umekaribisha hatua ya pande zote katika mzozo nchini humo kutekeleza wito wa kusitisha uhasama uliotolewa Agosti 8 kwa ajili ya maadhimisho ya sikukuu ya Eid Al Haj na kusema imesaidia kupunguza machafuko hasa katika mji mkuu Tripoli.
Umoja wa Mataifa na mashirika yake umelaani vikali shambulio la jana kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli ambalo limesababisha vifo vya takribani watu 44 na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa.
Umoja wa Mataifa na mashirika yake umelaani vikali shambulio la jana kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli ambalo limesababisha vifo vya takribani watu 44 na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO limelaani vikali shambulio dhidi ya gari la wagonjwa kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli ambalo limejeruhi wahudumu watatu wa a
Shirika la afya ulimwenguni, WHO limelaani vikali shambulio dhidi ya gari la wagonjwa kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli ambalo limejeruhi wahudumu watatu wa afya, mmoja wao hali yake ikiwa mbaya zaidi.
Nchini Libya maelfu ya wanawake, watoto na wanaume wamelazimika kufungasha virago na kukimbilia nje ya mji mkuu Tripoli kufuatia machafuko yanayoendelea katika eneo la Kaskazini la mji huo.
Ripoti kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, iliyochapishwa hii leo inasema mapigano ya kutumia silaha nzito na mashambulizi kutoka angani vimeendelea katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Libya, Tripoli na viungani.