Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika isipotumia fursa ya biashara mtandao, wengine wataitumia- Kituyi

Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kitui
Photo: UNCTAD
Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kitui

Afrika isipotumia fursa ya biashara mtandao, wengine wataitumia- Kituyi

Ukuaji wa Kiuchumi

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema nchi za Afrika zisipoanzisha majukwaa ya kufanya biashara mtandaoni, basi fursa hiyo itachukuliwa na mataifa mengine ambayo yameshajiimarisha kwenye sekta hiyo.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York,  Marekani  hivi karibuni.

Dkt. Kituyi amesema majukwaa hayo yamenufaisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo katika sekta mbalimbali na ndio maana..

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

 Kwa mantiki hiyo amesema..

(Sauti ya Dkt. Kituyi)

Ili kufanikisha hilo, Katibu Mkuu huyo wa  UNCTAD amesema wameandaa mkutano mwezi disemba mwaka huu huko Nairobi nchini Kenya ambako viongozi wa Afrika watajumuika na magwiji wa biashara ya mtandao ili kuweza kujifunza vyema jinsi ya kutumia mbinu hiyo kukuza uchumi Afrika katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.