Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCTAD na Ali Baba washirikiana kukwamua vijana

Wasichana na wavulana kutoka kituo cha uanagenzi wakijifunza kwa vitendo.
UNFPA/Roar Bakke (maktaba)
Wasichana na wavulana kutoka kituo cha uanagenzi wakijifunza kwa vitendo.

UNCTAD na Ali Baba washirikiana kukwamua vijana

Ukuaji wa Kiuchumi

Maendeleo ya teknolojia yanazidi kuleta nuru duniani ambapo Umoja wa Mataifa nao unatumia fursa ya kupitia wadau wake ili kuona maendeleo hayo yananufaisha watu wote ikiwemo vijana hususan wale wa pembezoni.

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezungumzia ushirikiano wake na kampuni ya Ali baba katika kuinua uwezo wa vijana wa Afrika kwenye kutumia majukwaa ya kieletroniki kuuza bidhaa zao.

Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amezungumzia mradi huo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Amesema wamanzisha mradi huo na Jack Ma, kiongozi wa kampuni ya Ali Baba ambapo vijana kutoka Afrika wanakwenda jimboni Hangzhou kujifunza jinsi ya kujenga majukwaa ya biashara mtandaoni.

Dkt. Kituyi amesema majukwaa ya aina hiyo yanasaidia kupunguza gharama za matangazo.

Halikadhalika faida nyingine ni kwamba inawezesha wafanyabiashara kufikia masoko  ya kimataifa.

Image
Vijana wajasiriamali nchini Tanzania. Picha: UM/Video capture