Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shamubilzi lingine moja tu Hodeidah litakuwa janga lisilozuilika: OCHA

Mtu anachota maji katika daraja lililobolewa kwa mashambulizi Yemen. OCHA unasaidia watu walio katika hali kama hiyo 2017
Picha ya OCHA/Giles Clarke
Mtu anachota maji katika daraja lililobolewa kwa mashambulizi Yemen. OCHA unasaidia watu walio katika hali kama hiyo 2017

Shamubilzi lingine moja tu Hodeidah litakuwa janga lisilozuilika: OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Bandari muhimu nchini Yemen ya Hodeidah ambayo imekuwa ikiandamwa na mashambulizi kutoka kwa vikosi vinavyounga mkono serikali kwa wiki kadha, sasa iko taabani na huenda shambulio linguine moja tu la anga likuka kuwa janga lisilozuilika, kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, OCHA.

Ameongeza kuwa mashambulizi ya juzi, jana na leo yamesambaratisha miundombinu ikiwemo mifumo ya maji, kituo cha afya uzazi na maabara.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Sana’a hii leo , Lise Grande amesems "kwa wiki kadhaa  sasa tumekuwa tukifanya kila tuwezalo ili kusaidia mamia kwa maelfu ya watu wanaoishi katika mji wa Hodeidah na viunga vyake, hata hivyo,  mashambulzi haya yanawaweka watuwaasiona hatia katika hatari kubwa“.

Ameongeza kuwa bandari ya Hodeidah  ni njia kuu na muhimu ya kuingiza chakula na misaada mingine ya kibinadamu katika taifa hilo lililoghubikwa na vita na limekuwa mikononi mwa waasi wa Houthi ambao wamekuwa wakipigana na serikali kwa msaada wa muungano unaoongozwa na Saudia tangu mwishoni  mwa 2014.

Jumla, watu milioni 22 - au asilimia 75 ya wakazi wa Yemeni  wanahitaji aina fulani ya msaada wa kibinadamu au ulinzi, ikiwa ni pamoja na wengine takriban milioni 8.5 ambao hawajui wapi mlo wao ujao utatoka .

Majeshi ya muungano yalihamia Hudaydah mwezi juni, lakini jitihada za kidiplomasia zilizoongozwa na Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Yemen, Martin Griffiths, zimesaidia kuzuia uvamizi wa kijeshi katik  mji huo, wakati pande kinzani zikiwa katika mazungumzo ya  uwezekano wa muafaka ambao utawezesha makundi ya  wapiganaji kuondoka.


Hata hivyo,  wahudumu katika vituo vya afya wameripoti kwamba watu  328 wamejeruhiwa na karibu 50 waliuawa wakati wa mapigano  mwezi huu wa saba.

Tangu kuanza kwa mashambulizi ya  kijeshi ya hivi karibuni" Bi.  Grande amesema OCHA na "washirika wa masuala ya kibinadamu wamekuwa wakitoa msaada wa chakula, maji, vifaa vya dharura, fedha na huduma za afya. Ameongeza kuwa” asilimia 80 ya watu waliofueushwa na mapigano wamepokea aina fulani ya msaada.”

Grande amesema  ukiwa ni moja ya kitovu cha mlipuko mkubwa  wa kipindupindu kilichozuka mwaka jana  nchini Yemen, ugonjwa huo sasa uko katika iji ya namajimbo ya jirani , na kuharibiwa kwa mfumo wa maji, usafina vituo vya afya kuna weka mashakani juhudi zote ambazo tumekuwa tukijitahidikuzifanya .