Utoro usipodhibitiwa lengo la elimu itakuwa ndoto Tanzania:
Utoro mashuleni ni moja ya tishio kubwa la kutotimiza lengo namba nne la maendeleo endelevu lihusulo elimu kama hautodhibitiwa nchini Tanzania. Sasa serikali imeamua kulivalia njuga sula hilo kwa kampeni ya mkoa kwa mkoa na mkono wa sheria.
Kampeni hizo ni za kuihamasisha jamii kuelewa umuhimu wa elimu, kuwafikisha mahakamani wazazi wasiohimiza watoto kwenda shule au wanaowafanyika kazi watoto badala ya kuwapeleka shule , lakini pia maandamano ya amani kama yaliyofanyika mkoani Tabora wiki hii na kuhususisha viongozi wa serikali, waalimu, wazazi na wahusika wakuu ambao ni wanafunzi
SAUTI ZA WANAFUNZI
Je hizo ndio sababu pekee za utoro mashuleni? Adda Ezra ni mwalimu wa shule ya sekondari Ukombozi mkoani Taabora
SAUTI YA MWALIMU ADDA EZRA
Serikali ya Tanzania inasema wazazi wanawajibu mkubwa kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shule hivyo imetoa halahala kwa wazazi wasio wajibika kwani mkono wa sheria utawafuata na wameagizwa na mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri anayeongoza kampeni hiyo kutii amri la sivyo
SAUTI YA AGGREY MWANRI
Naye mwanasheria mkuu wa mkoa tabora Richard Lugomela akafunguka kuhusu adhabu
SAUTI YA RICHARD LUGOMELA
Kampeni hiyo ya kupinga utoro shuleni na utumikishwaji wa watoto imebeba kaulimbiu “kamata weka ndani kwa kutotii amri halali” inalenga kuinua kiwango cha elimu mkoani humo, kukomesha utoro na kuhakikisha lengo la elimu kitaifa linatimia ifikapo 2030. Wanafunzi zaidi ya 11,000 wa shule za msingi na sekondari ni wameorodheshwa kuwa ni watoto sugu mkoani Tabora.