Ingawa tumepiga hatua Tanzania bado tuna safari ndefu kutimiza lengo la elimu:Kalage

10 Julai 2019

Tanzania imepiga hatua kubwa katika safari ya utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s hususani katika lengo namba 4 la elimu katika upande wa usajili watoto shuleni lakini safari ya kutiza lengo hilo bado ni ndegu kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya Haki Elimu.  

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa unaotathimini hatua zilizopigwa n anchi mbalimbali katika utekelezaji wa malengo hayo John Mhando Petro Kalage kutoa asasi ambayo ni mdau mkubwa wa elimu nchini Tanzania yenye kazi  kubwa ya kufuatilia miakakati ya será za elimu nchini humo, amesema kutimiza lengo la elimu sio usajili tu bali pia elimu wanayoipata watoto na kuhakikisha wanamaliza shule na ndio maana kazi yao kubwa ni

SAUTI YA JOHN KALAGE 

Ameongeza kuwa ni muhimu kujua chanzo cha matatizo yanayowafanya Watoto kutohudhuria au kumaliza shule kama ndoa za utotoni, mila na desturi, changamoto za miundombinu na nyingine nyingi na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa kushirikisha wadau wote la sivyo utimizaji wa lengo namba 4 la elimu Tanzania itakuwa ndoto

SAUTI YA JOH KALAGHE 

Jukwaa hilo la ngazi ya juu kuhusu  tathimini ya hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa SDG’s litakunja jamvi wiki ijayo.

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter