Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hadithi za wakimbizi wanaorejea kutoka Libya zitatia uchungu: Grandi 

Mama na mtoto wake nchini Libya. Picha: UNFPA

Hadithi za wakimbizi wanaorejea kutoka Libya zitatia uchungu: Grandi 

Wahamiaji na Wakimbizi

Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi, amesafiri usiku kucha hadi nchini Niger akiambatana na wakimbizi zaidi ya 100 wengi wakiwa wanawake na watoto, waliosafirishwa kutoka kwenye kituo walichokuwa wanashikiliwa nchini Libya. 


Hapa ni Tripoli kwenye kituo cha Trik Al Sikka kinachoshikilia wakimbizi , Grandi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa shirikala Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,  huku nyuso za furaha kwa wakimbizi  zikitamalaki na wengine wakikumbatia kuuagana kuashiria safari imeiva.

Grandi anesema


(SAUTI YA FILIPPO GRANDI)
“Kwa upande mmoja huu ni wakati mzuri sana kwa watu wanaoondoka , tunashuhudia kuondoka kwa idadi kubwa ya wakimbizi kutoka katika kambi hii wakipelekwa Niger, ambako wataanza mchakato wa kupewa makazi kwenye nchi zingine na tunatumai watafanikiwa. Na kwa upande mwingine, tulikutana na machungu, wakati mwingine kukata tamaa, kwa wale wanaosalia. Na hali katika kizuizini hiki ni mbaya sana hususan kwa upande wa wanaume.”

Image
Wakimbizi waliokuwa wanashikiliwa Libya. Picha: UNHCR


Sasa majina ya wanaosafiri yanaitwa, wanasubiri wakiwa na masanduku yao kuanza kuingia kwenye basi kuelekea uwanja wa ndege. Mkuu wa UNHCR Bwana Grandi akafunguka


(SAUTI YA FILIPPO GRANDI)


“Zaidi ya yote ni baadhi ya haditi unazokumbana nazo mahali kama hapa. Hadhidi za majinamizi ya safari walizopitia , wanawake wengi wamebakwa, wengi wamejifungua walipowasili ,ni dhahiri walibakwa wakiwa safarini , sababu wako peke yao, na habari za kusikitisha za wale ambao labda wanamatumaini kidogo au hawana fursa kabisa ya kupatiwa makazi, hivyo inabidi wafikirie ustaarabu mwingine , lakini kuishi hapa ni ngumu.”


Sasa wakimbizi hao wanaingia kwenye ndege tayari kwa kuondoka , wakitabasamu kwa matumaini, Grandi anakumbusha

Image
Wakimbizi na wahamiaji wanalala sakafuni katika kituo cha kizuizini cha Tariq al-Sikka huko Tripoli, Libya. © UNHCR / Iason Foounten


(SAUTI YA FILIPO GRANDI)
“ Tusisahau kwamba vituo kama hivi vipo vingi Libya, baadhi tuna fursa vingine fursa bado ni vgumu, hivyo kazi ya kishujaa inayofanywa na wafanyakazi wetu hapa ni vita kubwa sana dhidi ya vikwazo vyote, kila siku. siku saba kwa wiki.”


Hatimaye wakimbizi hao 121 wengi kutoka Eritrea wamewasili Niamey Niger na baada ya hapo watapelekwa kupata makazi nchi zingine kupitia mpango mpya wa kimataifa.


Kwa mujibu wa UNHCR hivi sasa kuna wahamiaji na wakimbizi 6500 wanaoshikiliwa katika vituo rasmi nchini Libya wakiwemo watu 2700 ambao mazingira yao yanaitia hofu UNHCR.