UN  yakaribisha tangazo la wataliban Afghanistan

9 Juni 2018

Ghasia sasa zimetulia Afghanistan kuelekea Eid El Fitr

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres  amekaribisha tangazo la wataliban la kusitisha kwa muda hujuma dhidi ya serikali ya Afghanistan kwa kipindi cha  siku tatu za  sherehe za Eid El Fitri.

Tangazo hilo la Taliban nalo linatokana na lile la serikali ya Afghanistani kuwa inaanza sitisho la mapigano la siku saba kuelekea sikukuu hiyo.
 
Katibu Mkuu amesema anaamini kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwenye mzozo huo na kwamba suluhu ya kisiasa ndio inayoweza kumaliza machungu ya raia wa Afghanistan.
 
Halikadhalika amesihi pande zote husika nchini humo zitumie fursa hii na kusongesha mchakato unaoongozwa na raia wa Afghanistan wenyewe wa amani.

Amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake umeazimia kusaidia raia wan chi hiyo na serikali yao kwenye ari hiyo.
TAGS: Afghanistan, Eid El Fitr.

________________________________________

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter