Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katu hatutowasahau waliopoteza maisha kulinda amani duniani

Hafla ya kuweka shada ya maua kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha yao wakati wakitekeleza majukumu yao.
Picha: UM/Mark Garten
Hafla ya kuweka shada ya maua kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha yao wakati wakitekeleza majukumu yao.

Katu hatutowasahau waliopoteza maisha kulinda amani duniani

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa umesema walinda amani waliopoteza maisha wakihudumu kwenye maeneo hatarishi zaidi duniani, walijitoa mhanga ili kuhakikisha dunia inakuwa pahala salama zaidi. 

Ndani ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, wawakilishi wa nchi wanachama wa umoja huo, maafisa wa ulinzi wa amani na wageni waalikwa wakisubiri kwa hamu halfa ya siku ya walinda amani, iliyofanyika hii leo.

Tukio lilianza kwa Katibu Mkuu Antonio Guterres kuweka shada la maua kwenye eneo maalum…kukumbuka walinda amani 3700 waliopoteza maisha tangu kuanza kwa huduma hiyo mwaka 1948.

Mwaka jana pekee 61 waliuawa wakiwemo walinda amani 14 kutoka Tanzania, mmoja hadi sasa hajulikani alipo.

Na ndipo Katibu Mkuu akasema ..

“Walijitoa mhanga Maisha yao ili kulinda maisha ya wengine. Tunasalia daima na deni na siku zote tutawakumbuka.”

(Picha:UNNewsKiswahili/Assumpta Massoi)
Tutawakumbuka daima!

Na kwa familia zilizopoteza ndugu zao Bwana Guterres amesema..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Tunatambua jinsi familia na marafiki wa walinda Amani wote walivyojitoa, lakini zaidi kwa wale ambao hawakurejea nyumbani.”

Katibu Mkuu akaenda mbali zaidi kusema kuwa Umoja wa Mataifa utahakikisha unafanya ulinzi wa Amani unakuwa thabiti, salama na fanisi kupitia mpango wa utekelezaji wa ulinzi wa Amani uliozinduliwa mwaka jana.

Miongoni mwa walioshiriki tukio hili ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero.

(Sauti ya Balozi Modest Mero)