Epuka mafuta mabaya kwenye chakula- WHO

4 Mei 2018

Umoja wa Mataifa unataka walaji kuepuka matumizi ya mafuta mabaya ambayo huganda kwenye mishipa ya damu kwenye moyo na kusababisha magonjwa ya moyo.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema mafuta hayo mabaya ni pamoja na yale yanayotengenezwa viwandani kwa kuongeza hydrogen ili kunogesha chakula na pia kuwezesha chakula kuhifadhiwa kwa muda mrefu au Trans Fat.

Mafuta mengine ni yale yanayopatikana kwenye maziwa ya ng’ombe, jibini,  samaki aina ya Salmoni na vitafutwa vitamutamu vinavyookwa kama vile keki.

Kwa mujibu wa WHO mafuta hayo husababisha watu milioni 17 kufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo.

Chakula ambacho kinasababisha utipwatipwa. Picha: WHO
Chakula ambacho kinasababisha utipwatipwa. Picha: WHO

Ni kwa mantiki hiyo WHO imepitisha mwongozo mpya unaotaka watu kupunguza kwa asilimia 10 matumizi yao ya mafuta hayo.

Dkt. Francesco Branca ni Mkurugenzi wa masuala ya lishe WHO.

(Sauti ya Dkt. Francesco Branca)

 “Iwapo kweli tunaka kuondoa kabisa hatari ya mafuta haya, lazima kuwe na hatua thabiti za serikali kuhakikisha kwamba bidhaa zinazotengenezwa hazitumii mafuta yatokanayo na mboga ambayo yameongezewa hydrojeni kiwandani. Hata hivyo hatua ya baadhi ya nchi kuondoa mafuta hayo bado hakujatambuliwa vyema na mlaji. Kwa hiyo wazalishaji wanaweza kutumia aina nyingine ya mafuta yenye viambatano hivyo hivyo ili mlaji apate kitamutamu kizuri kisicho na mafuta mabaya.”

Hata hivyo rasimu hiyo ya mwongozo huo kabla ya kuchapishwa mwakani, utaleta pamoja wadau ili wajadili na kuhakikisha unakidhi matakwa ya kikanda.
 

 

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter