Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warohingya wajiandaa kabla ya hatari ya monsuni

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar Bangladesh
©Caroline Gluck/UNHCR
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar Bangladesh

Warohingya wajiandaa kabla ya hatari ya monsuni

Msaada wa Kibinadamu

Nchini Bangladesh shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linashirikiana na warohingya waliosaka hifadhi humo katika kuandaa vema makazi na uhifadhi wa chakula wakati huu ambapo msimu wa pepo za monsuni unabisha hodi.

 Nat

Katika makazi ya warohingya huko Cox’s Bazar tayari mvua zilizonyesha zimetwamisha maji ambayo watoto wamegeuza kuwa ni mchezo.

Hali ya mazingira ni duni na WFP ina hofu hali ya mazingira na chakula itakuwa mbaya zaidi mvua za monsuni zitakapoanza rasmi.

Peter Guest ni mratibu wa masuala ya dharura ya WFP katika eneo la Cox’s Bazar

(Sauti ya Peter Guest)

“Tunahitaji kuhakikisha iwapo wakati utakapowadia vituo vyetu vya kugawa chakula vitaweza kufikiwa. Kwa hivyo kuna kazi inayoendelea ya kurekebisha miinuko ili kuhakikisha kuwa walengwa wanaweza kufikia vituo mgao wa chakula.”

Miongoni mwa kazi zinazofanyika ni kuzibua mifereji, kazi inayofanywa kwa matrekta lakini pia kwa wakimbizi wenyewe ambao wanachimba mitaro na kufukia mabomba.

SFX: Matreka na majembe

(Sauti ya Peter Guest)

“ Kazi ya kushughulikia mahali hapa inasonga mbele ambapo tunatayarisha sehemu ya wakimbizi ambao sasa wako katika maeneo hatari  ya kutokea mafuriko na watahamishiwa katika maeneo ya hapa upande wa magharibi mwa kambi ambako inaonekana kama  ni eneo salama”.

WFP inasema kwa sasa inahitaji dola millioni 213 kuweza kuhakikisha usalama wa wakimbizi zaidi ya 800,000 wa Rohingya walioko Cox’ Bazar kwa kipindi  kilichosalia cha mwaka wa 2018.

Serikali ya Bangladesh ilitoa eka 800 za ardhi za kuwahamishia  wakimbizi 30,000 wa Rohingya wa Cox’s Bazar ambapo WFP inasema  eneo hilo limejaa milima na mabonde, lakini ikaongeza kuwa  ni eneo dogo tu la ardhi ambalo linaweza kutumiwa kwa kilimo.