Vietnam yatoa msaada kwa dola 50,000 kusaidia shughuli za WFP huko Cox’s Bazar.

11 Februari 2019

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP leo limekaribisha mchango mpya wa dola 50,000 kutoka Vietnam kwa ajili ya shughuli za mpango huo katika kambi za wakimbizi wa Rohingya huko Cox’s Bazar nchini Bangladesh.

Taarifa ya WFP iliyotolewa leo huko Dhaka, Bangladesh imememnukuu mwakilishi wa WFP nchini humo Richard Ragan akisema kuwa, “tunawashukuru sana Vietnam kwa kujitokeza kuwasaidia watu wanaoishi katika kambi za Cox’s Bazar. Hii inasalia kuwa hali ya dharura na msaada endelevu kutoka jumuiya ya kimataifa ni muhimu sana kama tunataka kuendelea kutoa msaada wa kibnadamu ambao unahitajika sana.”

Akitangaza mchango huo wakati wa ziara yake nchini Bangldesh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, wa Vietnam Nguyen Quoc Dzung amesema, “ingawa huu ni mchango mdogo, tunatumai utasongeza usaidizi.”

Huu ni mchango wa kwanza wa Vietnam kwa shughuli za WFP nchini Bangladesh na wanaungana na nchi nyingine ambazo zimeahidi usaidizi wao kwa shughuli zinazoendelea Cox’s Bazar tangu wakimbizi walipoanza kuingia mwezi agosti mwaka 2017.

Katika kambi za Cox’s Bazar, WFP inatoa msaada wa chaula kwa Zaidi ya wakimbizi 870,000 kwa mwezi. Pia WFP inatoa msaada wa lishe na usaidizi mwingine kwa jamii wenyeji kwa kuwasaidia watu walioko hatarini.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter