Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wanahitaji mazingira salama kazini :ILO

Wafanyakazi vijana wako katika hatari zaidi ya kujeruhiwa na kemikali na madawa mengine kwa sababu bado wanakua kimwili na kiakili
Picha na Maxime Fossat/ILO
Wafanyakazi vijana wako katika hatari zaidi ya kujeruhiwa na kemikali na madawa mengine kwa sababu bado wanakua kimwili na kiakili

Vijana wanahitaji mazingira salama kazini :ILO

Haki za binadamu

Wafanyakazi vijana kote duniani ndio walio katika hatari zaidi ya kujeruhuwa kazini kutokana na kemikali au madawa ya aina nyingine kwa sababu ya maendeleo yao ya kimwili na kiakili. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na shirika la kazi duniani  ILO, katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini , zaidi ya asilimia 40  ya viajana wote  walio katika ajira  ndio wanaojeruhiwa kazini wengi wakiwa na umri wa miaka 25.


ILO inasema hali hiyo inachangiwa na sababu nyingi ikiwemo umri wao hasa wa maendeleo ya kimwili na kiakili , kutokuwa na uzoefu wa kutosha na mafunzo, uelewa mdogo wa hatari zilizopo zinazohusiana na kazi na kukosa uwezo wa ushwawishi hali inayowafanya kukubli kazi ambazo ni za hatari na zenye mazingira mabaya.


Siku ya kimataifa ya usalama na afya kazini na siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto wameungana katika kampeni ya pamoja mwaka huu ili kuchagiza kuboresha usalama na afya ya vijana kazini na kukomesha ajira kwa watoto.
Kampeni hiyo imeaandaliwa ili kuchagiza mafanikio ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s, ikiwemo kupigania haki za wafanyakazi, kupigia upatu usalama katikamahali pa kazi na kuwalinda wafanyakazi ifikapo 2030, pia kukomesha ajira ya watoto katika mifumo yote ifikapo 2025.

Mwanahabari kijana Rashid Malekela anazungumza na vijana wenzake wa Mwanza Network studio
Mwanza Youth reporter
Mwanahabari kijana Rashid Malekela anazungumza na vijana wenzake wa Mwanza Network studio


Ili kutimiza haya ILO inasema ni lazima kuchukua msimamo mkali kwa lengo la kukomesha ajira kwa watoto na kuchagiza utamaduni wa kuzuia  na usalama na afya makazini kwa ajili ya kuboresh na kuimarisha maeneo ya kazi kote duaniani kwa mustakhbali wa wote.
Takwimu za ILO zinaonyesha kwamba zaidi ya vijana milioni 375 wenye umri wa kati ya miaka 15-24 wanafanya kazi za hatari.


Maadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini mwaka huu 2018 yanahimiza umuhimu wa changamoto hizi na kuboresha usalama na afya ya vijana kazini, sio tu kwa sababu ya kuchagiza ajira bora kwa vijana bali pia kujiunga na juhudi za kupambana na ajira ya watoto katika mifumo yote.