Waogiek tunajikongoja Kenya,serikali tushikeni mkono: Prengei
Wakati jukwaa la kimataifa la watu wa asili likiwa katika wiki ya pili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, watu wa asili kutoka jamii ya Ogiek nchini Kenya wanasema wanakimbiza treni ya SDGs lakini bila mkono wa serikali kuikamata itakuwa mtihani.