Chuja:

Watu Asili

Watu Asili kushiriki na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai: Burundi

Kongamano la watu asili kutoka  eneo la Maziwa makuu  barani Afrika limehitimishwa mjini  Bujumbura Burundi . Lilijikita katika jinsi Jamii hiyo wanavyoweza kushiriki na  kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo wanakoishi.

Jamii hiyo imekuwa inanyooshewa kidole kwa kuhusika na sehemu kubwa katika uharibifu wa mazingira, madai ambayo wanayakana wakitaja kwamba mazingira ni sehemu ya maisha yao.

Kutoka bujumbura , Muandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA amefuatilia kongamano hilo na kuandaa makala hii.

Sauti
4'4"