Dola bilioni 2 zaahidiwa leo kwa ajili ya yemen: Guterres

3 Aprili 2018

Ahadi ya dola zaidi ya bilioni 2 zimetolewa leo kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu nchini Yemen. Akitangaza jumla ya ahadi hizo kwenye mkutano wa kimataifa wa harambee ya Yemen mjini Geneva Uswis , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza kuwa rasilimali ni muhimu sana , lakini hazitoshi, cha msingi ni kuhakikisha zinawafikiwa watu wenye uhitaji, na ili hilo lifanikiwe inahitajika fursa ya kufika kila kona nchini Yemen bila vikwazo.

Guterres amewashukuru wote waliojitoa kwa moyo na kuzitaka pande zote katika mzozo kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu na zaidi ya yote kuwalinda raia. Kwa mantiki hiyo amesisitiza unahitajika mchakato wa kisiasa utakaopelekea suluhu ya kisiasa.

Mkutano huo ulioandaliwa na serikali ya Uswis na Sweden umewaleta pamoja wadau mbalimbali, ukiwemo Umoja wa Mataifa na mashirika yake, mashirika ya kimataifa, na wahisani ili kusaka dola takriban bilioni 3 zinazohitakika kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya watu zaidi ya milioni 13 Yemen kwa mwaka 2018.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter