Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi kambi za Tanganyika DRC hali yao taabani:Lowcock

Wakimbizi wa Burundi wakiwa kwenye fukwe za Ziwa Tanganyika wakisubiri majaliwa yao. (Picha: UNHCR/F.Scoppa)

Wakimbizi kambi za Tanganyika DRC hali yao taabani:Lowcock

Haki za binadamu

Msaidizi wa Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na kuratibu misaada ya dharura na waziri wa biashara ya nje na ushirikiano wa maendeleo wa Uholanzi, wamesema hali ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ni mbaya sana na hatua za haraka zahitajika kunusuru watu hao. 

Viongozi hao Mark Lowcock na Sigrid Kaag wameyasema hayo walipozuru kambi za wakimbizi wa ndani za Katanika na Kalungua zilizo Kalemie jimboni Tanganyika na kusikia hadhithi za madhila yanayowakabili wakimbizi hao.

(VOX POPS ZA WAKIMBIZI)

Bwana Lowcok akafunguka..

(SAUTI YA LOWCOK)

“Kitu kinachohitajika kuliko vyote ni amani na usalama na mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO unafanya kazi nzuri , lakini wanasiasa wan chi hii na watu wenye sialaha wanahitaji kukomesha mzozo na mapigano, hali ni mbaya sana na tatizo kubwa tulilonalo ni upungufu wa fedha kukidhi mahitaji ya watu hawa.”

Na kwa mantiki hiyo

(SAUTI YA LOWCOK)

“Tunaomba dola bilioni 1.7 mwaka huu kwa ajili ya msaada wa kibinadamu congo, hiyo ni mara mbili ya tulivyoomba mwaka jana kwa sababu tatizo ni baya mara mbili.”

Tarehe 13 Aprili mwaka huu Umoja wa mataifa utakuwa na tukio maalumu la harambee mjini Geneva kwa ajili ya kusaidia DRC na nchi jirani.