Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo milioni 7 kila mwaka vitokanavyo na tumbaku havistahiki: WHO

Watu wengi waomeonywa kuhusu matumizi ya tumbaku.
WHO/ Regional Office for the Western Pacific
Watu wengi waomeonywa kuhusu matumizi ya tumbaku.

Vifo milioni 7 kila mwaka vitokanavyo na tumbaku havistahiki: WHO

Afya

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa mwuongozo mpya kuhusu ujukumu la sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku na kuonyesha jinsi zinavyoweza kupunguza mahitaji, kuokoa maisha na kupunguza gharama za huduma ya afya katika kutibu maradhi yatokanayo na bidhaa za tumbaku.

Muongozo huo umezinduliwa mjini Cape Town Afrika Kusini na mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedross Gebreyesus wakati wakikunja jamvi la mkutano wa 17 wa kimataifa kuhusu bidhaa za tumbaku uliowaleta pamoja mamia ya nchi wanachama wa WHO. Waziri wa afya wa Uganda Sarah Opendi ni miongoni mwa waliohudhuria.

(SAUTI YA SARAH OPENDI)

Hata hivyo anasema utekelezaji wa sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku unakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa makampuni na wauzaji wa bidhaa hizo kama sigara

(SAUTI YA SARA OPENDI)

WHO inasema watu milioni 7 hufariki dunia kila mwaka kutokana na maradhi yanayokanayo na matumizi ya bidhaa za tumbaku na imesisitiza katika upimaji maabara, kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto na kuhakikisha kila mwanachana anatia saini na kutekeleza mkataba wa kimataifa wa WHO kuhusu bidhaa za tumbaku.