Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusikubali kampuni za sigara zifadhili matukio ya michezo- WHO

Mwanaume akivuta sigara katika eneo lililotengwa kwa ajili ya wavuta sigara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani.
UN News/Yasmina Guerda
Mwanaume akivuta sigara katika eneo lililotengwa kwa ajili ya wavuta sigara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani.

Tusikubali kampuni za sigara zifadhili matukio ya michezo- WHO

Afya

Shirika la afya ulimwenguni, WHO linasihi serikali kote duniani kusimamia kwa kina sheria inayozuia kampuni za sigara kufadhili au kutangaza sigara kwenye matukio ya michezo yakiwemo yale ya mbio za magari na pikipiki.

Taarifa ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi inasema pamoja na serikali, shirika hilo linataka vyombo vinavyosimamia michezo hiyo ya mbio za magari na pikipiki zipitishe sera za kutokuwepo kwa tumbaku au sigara kwenye mashindano ikiwemo washiriki, washindani na hata timu zinazoshiriki zisifadhiliwe na kampuni za sigara.

Wito huo umekuja baada ya kampuni za tumbaku kuanzisha ubia mpya na timu za mashindano ya magari na pikipiki.

Mathalani kampuni ya tumbaku ya Uingereza, BAT ilitangaza hivi karibuni ubia mpya wa kimataifa na timu ya mbio za magari za Formula 1, McLaren ambapo timu hiyo itatumia nembo yenye maneno, “Kesho bora.”

Katika tangazo lake kuhusu ubia huo huo wa miaka kadhaa, BAT imedokeza kuwa itaweka jukwaa la kimataifa kusongesha mbele bidhaa mpya ikiwemo glo, ambaoy ni tumbaku iliyochomwa.

WHO inasema kuwa, “taarifa hiyo inadokeza nia ya kampuni hiyo ya kuhamasisha matumizi ya tumbaku.”

Mwanaume akivuta sigara pembezoni mwa barabara katika eneo la vijijini Nepal.
World Bank/Aisha Faquir
Mwanaume akivuta sigara pembezoni mwa barabara katika eneo la vijijini Nepal.

Kwa upande wake, kampuni ya kimataifa ya Philip Morris, PMI, yenyewe imeanzisha logo mpya, “Mpango wa shinda sasa,” itakayobandikwa kwenye magari ya Ferrari, pikipiki za Ducati ambazo awali zilikuwa zinatumia sigara ya Malboro.

WHO inasema kuwa upigaji marufuku wa kina wa matumizi ya sigara kufadhili au kutangazwa kunapunguza matumizi ya bidhaa za tumbaku ikiwemo miongoni mwa vijana.

Ibara ya 13 ya mkataba wa kimataifa wa kudhibiti tumbaku, WHO-FTC unataka nchi wanachama izuie kaw dhati au iweke vikwazo kwenye matangazo na ufadhili wa michezo kupitia tumbaku.

WHO inabainisha kuwa matangazo ya tumbaku huonekana kwenye ambazo zinatangaza michezo husika na pia kwa nchi mwneyeji zinazopokea matangazo ya michezo hiyo.

Kwa mantiki hiyo WHO inasihi serikali zitekeleze sheria za ndani za kuzuia matangazo au ufadhili wa michezo unaofanywa na kampuni za michezo.