Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

tumbaku

26 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kama ilivyopangwa. Alisema tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI [SENI] imeshachapisha majina ya wagombea na michakato mingine inaendelea.

Sauti
11'49"

31 JULAI 2023

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika masuala ya afya hususan mafanikio ya será za kudhibiti uvutaji sigara na tumbaku; elimu kwa watoto waliokosa fursa huko Kenya; nishati salama nchini Tanzania na ujumbe wa Romeo George mwanaharakati wa SDGs.

Sauti
12'44"

31 MEI 2023

Hii leo katika jarida Anold Kayanda anamulika kwa kiasi kikubwa siku ya kutokomeza matumizi ya tumbaku duniani halikadhalika hatua ya kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania.

Sauti
11'25"

26 MEI 2023

Jaridani hii leo tunaangazia ripoti kuhusu matumizi ya tumbaku na wakimbizi wa Sudan. Makala tunaangazia mauaji ya kimbari nchini Rwanda na mashinani tutakupeleka nchini Chad, kulikoni?

Sauti
14'21"
Shamba la mmea wa tumbaku nchini Kenya
© WHO

FAO yawasaidia wakulima wa tumbaku Kenya, kuhamia katika mazao mbadala

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeimarisha afya ya wakulima wa kaunti ya Migori. Hii ni baada ya kuzindua machi Mwaka huu mradi wa kilimo mbadala unaolenga kusitisha kile cha tumbaku. Kwa ushirikiano wa WHO na WFP, FAO inajivunia mafanikio kwani afya za wakulima wa Migori zimeimarika baada ya kuacha kilimo cha tumbaku na kukiongeza kipato chao.