Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa muhimu UM:

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa muhimu UM:

[caption id="attachment_324210" align="aligncenter" width="625"]barazayemenvita

Mustakhbali wa watu wa Yemen unasalia kuwa na umuhimu mkubwa wakati huu wakikabiliwa na zahma kubwa ya kibinadamu. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York hii leo.

Mwishoni mwa juma mashambulizi ya anga yaliarifiwa kukatili maisha ya watu 12 raia wakiwemo wanawake na watoto. Mratibu wa masuala ya kibinadamu Yemen, Jamie McGoldrick, ameelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi hayo ya anga katika nyumba na magari binafsi na kusema matukio ya hivi karibuni yanafanyiwa uchunguzi na ofosi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa zaidi ya miaka miwli muungano unaoiongozwa na saudia , ukijumuisha ndege za kivita umekuwa ukipambana na kundi la waasi la Houthi linalosaidiwa na Iran katika kupata udhibiti wa taifa hilo. Kwa mujibu wa Stéphane Dujarric:

"wadau wote wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen wataendelea kufanya kazi na pande zote ili kufikisha misaada kwa watu wa Yemen wakati huu wakikabiliwa na zahma kubwa ya kibinadamu. Ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kutopoteza mwelekeo wa madhila yanayowkabili mamilioni ya watu wasiojiweza, wanaume, wanawake na watoto wa yemen. Ameongeza kuwa mustakhbali wao unasalia kuwa muhimu sana kwa Umoja wa Mataifa.