Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa amani umejeruhiwa lakini unaweza kutibika-Mogae

Mkataba wa amani umejeruhiwa lakini unaweza kutibika-Mogae

Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ufuatiliaji na tathmini, (JEMC) Festus Mogae, amejibu wito wa kumtaka kujiuzulu.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Juba Sudan Kusini bwana Festus Mogae, amesema anatambua kwamba jamii haijaridhika na kazi ya JMEC, lakini ameelezea dhamira yake ya kusaidia utekelezaji wa mchakatio wa amani nchini humo.

(MOGAE CUT)

“Nafahamu kwamba Wasudan Kusini wengi hawaridhiki na utendaji wangu, lakini sidhani kwamba ndio nimeshashindwa kabisa, wakati huo ukifika , nitafanya maamuzi na kukata tamaa. Nitajitahidi, na kama nitafeli basi nitafeli, na kama kufeli kwangu kutasababisha nisihalalishwe basi na iwe hivyo. Ntasema nimejitahidi lakini nimeshindwa na ilikuwa vyema kujaribu. Amani na kuokoa maisha vinathamani kubwa ya kujaribu kuweka maisha yangu hatarini kwa ajili hiyo, ndio maana wengi wetu tuko hapa kwa matumaiani kwamba tutafanikiwa."

Festus Mogae amesema pia anafahamu kwamba mkataba wa amani umejeruhiwa , lakini amesisitiza bado unaweza kutibika kwa haja ya wadau na serikali kutumia fursa ya IGAD kufufua mchakato wa amani.