Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la Wiki- Songobingo, Sokomoko na Segemnege

Neno la Wiki- Songobingo, Sokomoko na Segemnege

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno songobingo, sokomoko na segemnege. Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Nuhu anasema Songobingo inatokea wakati ambapo hakuna uelewa wa kinachoendelea linatumika kuonyesha uzito wa jambo, na Sokomoko ni wakatia kuna matatizo ambayo yanaleta uzito kwa mtu au jamii na segemnege ni wakati mambo yamekaa ovyoovyo  na hayaeleweki. Aidha amesema maneno haya yana uradidi kwani kila neno lina maneno ya uradidi yanayofanana.