Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasiki:Guterres

Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasiki:Guterres

Bahari,  ardhi, misitu , maji na hewa tunayovuta ni mazingira yetu ambayo ni viungo muhimu katika mustakhbali dunia. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kuhusu siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 5 na kuongeza

(GUTERRES CUT 1)

“Bila mazingira bora hatuwezi kutokomeza umasikini au kuleta ustawi,

wote tuna jukumu kulinda maskani yetu pekee. Tunaweza kupunguza matumizi ya plastiki, tukapunguza kuendesha vyombo vya moto , tukapunguza kutupa vyakula  na tukaelimishana kuhusu kujali.”

Kauli mbiu yam waka huu ni kutangamana na asili, hivyo akasisitiza

(GUTERRES CUT 2)

Katika Siku ya Mazingira Duniani na kila siku hebu tuungane na asili

hebu tuthamini dunia inayotulinda.