Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eritrea lazima imwachilie huru mwandishi Isaak-UM

Eritrea lazima imwachilie huru mwandishi Isaak-UM

Serikali ya Eritrea ni lazima imwachilie huru mwandishi wa habari Dawit Isaak ambaye ametunukiwa tuzo ya hadhi kubwa ya uhuru wa vyombo vya habari , miaka 15 baada ya kukamatwa, amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa.

Bi Sheila B. Keetharuth ambaye ni mwakilishi maalumu wa hali ya haki za binadamu nchini Eritrea, pia ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo jimboni Asmara kuwaachilia bila masharti yoyote watu wote wanaoshuikiliwa kinyume cha sheria.

Amesisitiza kwamba uongozi wa Eritrea uache mara moja vitendo vya kuwakamata na kuwasweka rumande watu bila msingi wowote huku akikaribisha tuzo ya uhuru wa vyombo vya habari ya Guillermo Cano ambayo hutolewa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sanyansi na utamaduni UNESCO , aliyotunukiwa mwandishi Isaak kwa mwaka 2017.

Dawit Isaak, mwenye umri wa miaka 52, mwandishi wa habari, mtunzi wa riwaya na mwandishi wa vitabu alikamatwa na uongozi wa Eritrea katika msako uliofanyika Septemba 2001 kwa kuikosoa serikali.