Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafikisha misaada ya dharura kwa wakimbizi wa DRC walioko Angola

UNHCR yafikisha misaada ya dharura kwa wakimbizi wa DRC walioko Angola

Ndege iliyosheheni vifaa vya msaada imewasili Jumapili nchini Angola ili kuwasaidia watu zaidi ya 11,000 waliokimbia machafuko ya karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokeasia ya Congo DRC.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linalowasaidia watu wanaokimbia jimbo la Kasai DRC, ndege hiyo iliyowasili kutokea Dubai imebeba msaada wa vitu kama magororo ya kulalia, mahema, vyandarua vya mbu na vyombo vya kupikia.

Machafuko jimboni Kasai yalizuka katikati ya mwaka jana na maelfu ya wakimbizi wamekuwa wakimiminika Angola wakiwemo watoto 4000.