Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wavuvi wawakilisha utambulisho wa kisiwa cha Jeju

Wanawake wavuvi wawakilisha utambulisho wa kisiwa cha Jeju

Kisiwa cha Jeju ni kisiwa kikubwa  katika rasi ya Korea. Ni moja ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyotajwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kwa kuwa na maliasili ambazo zinavutia watalii na hasa mila na tamaduni za kikundi cha wanawake na wasichana kiitwayo "jeju haenyeo” ambao hukabiliana na bahari kuvua samaki. UNESCO tayari imeingiza mila hizi katika orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Kwa undani zaidi ungana na Selina Jerobon katika makala ifuatayo..