Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyumba 1140, shule, hospitali zimeharibiwa Mosul- UN-Habitat

Nyumba 1140, shule, hospitali zimeharibiwa Mosul- UN-Habitat

Tathimini iliyofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-Habitat kwa kushirikiana na mpango wa umoja huo wa makazi ya watu, imethibitisha kuwa uharibifu mkubwa Magharibi mwa Mosul nchini Iraq kufuatia machafuko yanayoendelea.

Taarifa ya tathimni hiyo inaeleza kuwa zaidi ya nyumba 1140 zimeharibiwa katika maeneo ya mji, shule navituo vya afya na miundombinu muhimu ya umma ikiwemo umeme, maji na huduma za kujisafi.

Tathimini iliyotumia picha za setilaiti na watafiti wa maeneo hayo imebaini kuwa uharibifu wa nyumba Magharibi mwa Mosul ni mara mbili na nusu kuliko mashariki mwa wilaya hiyo.

Akizungumzia tathimni hiyo, Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Lise Grande amesema uharibifu magharibi mwa Mosul ni mkubwa zaidi wa ule wa Mashariki hata kabla ya mapigano kuanza mjini humo.

Zaidi ya watu 300,000 wamefurushwa mjini humo, huku mamia kwa maelfu wengine wakitarajiwa kusaka hifadhi .