Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makumi ya askari, raia wauawa katika machafuko Sudan Kusini: Dujarric

Makumi ya askari, raia wauawa katika machafuko Sudan Kusini: Dujarric

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Suda Kusini UNMISS, umesema askari kadhaa wa jeshi la serikali SPLA wameuawa katika majibishano ya mapigano jana mjni Wau Kaskazini mwa nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani,msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric, amesema umoja huo umechukua hatua za kudhibiti machafuko hayo ambayo yalienea katika maeneo kadhaa ya Wau na kwamba.

( Sauti Dujarric)

‘‘Wenzetu walioko kwenye ujumbe wa kulinda amani walituma vikosi viwili vya doria katika eneo hilo leo. Waliona miili 16 katika hospitali na majeruhi etakribani 10. Watu 84 wamewasili katika kituo cha ulinzi wa raia cha UNMISS huko Wau, watu wengine karibu 3,000 wameripotiwa kuhamishiwa kwenye kituo kinachomilikiwa na kanisa katoliki wngi wao wakiwa ni wanawake na wasichana.''

Amesema doria inatarajiwa kuendelea hapo kesho Jumanne.

Taarifa kutoka UNMISS zinasema kuwa chanzo cha mapigano hayo ni hatua ya vikosi vya SPLA na vifaa vyake kuhamishiwa kusini mashariki mwa Wau juma lililopita.