Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yawapa fidia wahanga 297 wa uhalifu wa Katanga

ICC yawapa fidia wahanga 297 wa uhalifu wa Katanga

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC leo imetoa amri ya kuwafidia wahanga 297 wa uhalifu uliofanywa na Germain Katanga katika wilaya ya Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo Februari 24 mwaka 2003. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Mahakama imesema fidia hiyo si toshelezi kwa madhara waliyoyapitia waathirika bali ni ishara na itawapatia kila muathrika dola za kimarekani 250, pamoja na makazi, msaada kwa ajili ya shughuli za uzalishaji, elimu na kisaikolojia.

ICC imesema fidia hiyo ni matakwa na mahitaji yaliyowasilishwa mbele ya mahakama na waathirika wenyewe na itasimamiwa na mfuko wa ufadhili kwa ajili ya waathirika, TVF ulioanzishwa na ICC, baada ya mahakama kubaini kuwa Katanga ambaye ameshuhudia hukumu hiyo kwa njia ya video kutoka jela huko DRC, hana uwezo wa kifedha wa kuwafidia wahanga hao.