Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasikilizaji Vindakindaki watoa ya moyoni kuhusu umuhimu wa redio

Wasikilizaji Vindakindaki watoa ya moyoni kuhusu umuhimu wa redio

Juma hili dunia ikiwa imeadhimisha siku ya redio mnamo Februari 13, wasikilizaji hususani wale wanaotufuatilia kupitia tovuti mathalani Facebook, wamesema uwepo wa idhaa hii ni muhimu kwa kuwapasha habari za kitaifa na kimataifa , huku wengine wakitoa maoni yao juu ya nini cha kuboreshwa.

Wasikilizaji hao ambao walitoa namba zao ili kuzungumza na kueleza hisia zao katika kuadhimisha siku ya redio duniani, maoni yao yamejikita zaidi katika namna wanavyonufaika na redio kwa ujumla na kisha idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa.

( SAUTI ZA WASIKILIZAJI)