Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Herve Ladsous kuondoka UM mwisho wa Machi mwaka huu

Herve Ladsous kuondoka UM mwisho wa Machi mwaka huu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  amesema mchakato wa mabadiliko katika sekta ya ulinzi na usalama ya Umoja wa Mataifa unaendelea kama alivyoahidi kutoa kipaumbele katika upande huo.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne Katibu Mkuu amesema katika kuhakikisha mabadiliko hayo ameamua kuanzisha timu ya ndani ya tathimini inayoongozwa na Bwana Tamrat Samuel. Timu hiyo itawasilisha mapendekezo kwa Katibu Mkuu ifikapo Juni 2017 ili kuanza mchakato wa majadiliano nan chi wanachama na pande zingine husiaka na hatimaye kuchukua hatua muafaka.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Katibu Mkuu ameamua kuongeza muda wa majukumu ya maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wanaofanya kazi katika idara ya ulinzi na usalama kwa mwaka mmoja zaidi hadi Aprili Mosi 2018.

Maafisa hao ni pamoja Bwana Jeffrey Feltman, ambaye ni msaidizi wa Katibu mkuu katika masuala ya siasa, Bwana Oscar Fernandez-Taranco Katibu mkuu msaidizi wa masuala ya msaada wa ujenzi wa amani na Bwana Atul Khare msaidizi wa Katibu mkuu kwa ajili ya usaidizi wa mashinani.

Ameongeza kuwa Hervé Ladsous, ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani amemuarifu katibu Mkuu kuwa hatokuwepo kuendelea na jukumu lake baada ya muda wa sasa kumalizika Machi 31 mwaka huu. Guterres amemshukuru kwa huduma yake kwa Umoja wa mataifa na juhudi za bila kuchoka katika mausla ya ulinzi wa amani . Katibu Mkuu amesema anapanga kumteua

Jean-Pierre Lacroix, kuchukua nafasi ya Ladsous kwa mwaka mmoja kuanzia April mosi mwaka huu. Lacroix, hivi sasa ni mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kwenye wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa.