Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 100 wasadikiwa kufariki dunia kwenye mapigano DRC

Watu 100 wasadikiwa kufariki dunia kwenye mapigano DRC

Zaidi ya watu 100 wanaaminika kuuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, katika mapigano baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kikabila. Amina Hassan na taarifa kamili

(TAARIFA YA AMINA)

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa wanamgambo wapiganaji walipigwa risasi kwenye jimbo la kati la Kasai na wanajeshi wa serikali wa FARDC, ingawa wanamgambo hao walikuwa wamejihami kwa mapanga na mishale.

Mapigano hayo yalizuka kwenye mji wa Tshimbulu. Liz Throssell ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA LIZ THROSSELL)

"Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali wanajeshi wa FARDC walipoona wanamgambo waliojihami kwa mapanga na mishale, waliwafyatulia risasi bila kubagua. Wanawake 39 wameripotiwa kukumbwa katika mapigano hayo na ni miongoni mwa waliopoteza maisha."

Ofisi ya haki za binadamu imelaani matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na vikosi vya serikali dhidi ya wanamgambo wa kikabila , lakini pia imezungumzia kupinga kitendo cha wanamgambo hao kuwaingiza watoto katika kmapigano ya kivita.