Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaidizi wa WFP umeleta nuru kwa watoto wa Yobe na Borno- WFP

Usaidizi wa WFP umeleta nuru kwa watoto wa Yobe na Borno- WFP

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP amesema usaidizi wa kifedha kwa watu walioathiriwa na mzozo kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeleta matumaini makubwa ikiwemo kwa watoto ambao tayari utapiamlo ulianza kuwaletea madhara. Taarifa kamili na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Amesema hayo huko Damaturu nchini Nigeria baada ya kutembelea kambi ya Pompomari inayohifadhi wakimbizi wa ndani waliokimbia majimbo ya Yobe na borno kutokana na mashambulizi ya Boko Haram.

Bi. Cousin amesema WFP imekuwa ikiwapatia fedha kupitia simu zao za rununu ambazo wanatumia kuchochea shughuli za kujikwamua kimaisha na kuimarisha familia zao huku watoto na wajawazito wakipatiwa msaada wa vyakula vyenye virutubisho.

Mathalani hivi sasa amesema watoto ambao mwezi Novemba mwaka jana hawakuweza kutembea kabisa, sasa wanatembea kutokana na usaidizi huo.

Hata hivyo amesema bado usaidizi unahitajika hivyo jamii ya kimataifa hivyo wasisubiri watoto wafariki dunia kwa njaa bali watoe misaada kwa wakati.