Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya 10 wauawa kwenye shambulio la bomu Mogadishu:UNSOM

Zaidi ya 10 wauawa kwenye shambulio la bomu Mogadishu:UNSOM

Watu zaidi ya 10 wameuawa Jumatano mjini Mogadishu Somalia katika shambulio la bomu. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa taarifa ya mpango wa Umoja wa mataifa nchini Somalia UNSOM iliyoandikwa kwenye mtandao wake wa Twitter , imelaani vikali shambulio hilo liliofanyika kwenye hotel ya Dayax baada ya gari lililokuwa na bomu kuingia kwenye gate la hoteli hiyo na kulipuka mapema Jumatano.

Watu takribani 15 wameuawa wakiwemo washambuliaji wa kujitoa muhanga na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al-Shaababb limekiri kuhusika na shambulio hilo na UNSOM inasema , ukatili wa itikadi kali asilani hautoshinda Somalia huku ikitoa wito wa kufikishwa kwenye mkono wa sheria wahusika.

Kundi la Al-Shaabab kwa muda limekuwa likidhibiti eneo kubwa la Somalia hadi mwaka 2011 lilipofurushwa mjini Moghadishu na vikosi vya muungano wa Afrika vinavyolinda amani nchini humo AMISOM.