Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama ungeni mkono ICC isisambaratike- Zeid

Wanachama ungeni mkono ICC isisambaratike- Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kuendelea kuunga mkono uwepo wa chombo hicho wakati huu ambapo baadhi ya nchi zinaendelea kujitoa.

Akizungumza huko The Hague, Uholanzi kwenye mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma ulionzisha ICC, Zeid amesema kujitoa kwa baadhi ya nchi kunaonekana kuwa na lengo la kulinda viongozi wao dhidi ya mashtaka.

Amesema anasikitishwa na hali ilivyo kwani nchi za Afrika zimekuwa msingi wa mahakama hiyo, lakini anatiwa moyo kuwa Botswana, Cote d’Ivoire, Nigeria, Malawi, Senegal, Tanzania, Zambia na Sierra Leone zimesema zitaendelea kuwa wanachama.

Zeid ametoa kauli hiyo wakati huu ambapo yaelezwa Urusi ina mpango wa kujitoa, wakati nchi tatu za Afrika; Burundi, Afrika Kusini na Gambia tayari zilishatangaza kujitoa.