Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinga na huduma za afya zidumishwe ili kutokomeza kisukari-Ban

Kinga na huduma za afya zidumishwe ili kutokomeza kisukari-Ban

Ikiwa leo ni siku ya kisukari duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni muhimu kujikita katika kinga na kuimarisha huduma za afya ili kuwasaidia watu zaidi ya watu milioni 200 duniani wenye kisukari. Flora Nducha na maelezo kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Katika ujumbe wake kuhusu siku hii, Ban amesema ugonjwa wa kisukari unaongoza katika kusababisha uono hafifu na upofu kwakuwa mabadiliko hayo yahana maumivu na ni ya taratibu na hivyo watu hugundua tatizo pale uono wao unapotatizika.

Amesema mgonjwa anapofikia hatua hii inakuwa vigumu kurejesha au kuimarisha uono na hivyo akasema watu wenye ugonjwa wa kisukari waweke utaratibu wa kupima macho mara kwa mara kwa wataalamu.

Nchini Tanzania, takwimu za serikali za mwaka 2012 zianonyesha kuwa asilimia tisa ya wakazi wa taifa hilo wana ugonjwa wa kisukari. Rachel Musese ni tabibu msaidizi katika kliniki iitwayo Star of Jerusalem, Kagera Tanzania.

( SAUTI RACHEL)