Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo mpya wahitajika kuboresha ajira zisizo maalum- ILO

Mfumo mpya wahitajika kuboresha ajira zisizo maalum- ILO

Shirika la kazi duniani, ILO limesema marekebisho ya mifumo pamoja na sera yanahitajika ili kuboresha ubora wa ajira zisizo maalum zinazoongezeka kila uchao. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

ILO imesema hayo katika ripoti mpya iliyochapishwa leo ikipatiwa jina; ajira zisizo rasmi ulimwenguni, kuelewa changamoto na kuweka matumaini.

Ripoti imebaini ongezeko la ajira za aina hiyo, ikiwemo zile vibarua, ukandarasi, kujiajiri, ajira za muda na kwamba kunaibuka changamoto ikiwemo waajiriwa kutokuwa na uhakika juu ya mustakhbali wa ajira zao huku wakipata malipo kiduchu.

Mwandishi wa ripoti hiyo Janine Berg amesema wametoa mapendekezo manne ikiwemo..

(Sauti ya Janine)

“Kufanya marekebisho ya kisera, ikiwemo sera za kuhakikisha huduma sawa miongoni mwa wafanyakazi bila kujali mikataba yao, mfano kuwapatia wafanyakazi wenye ajira zisizo maalum  maslahi sawa na wafanyakazi wenye mikataba ya kudumu.”