Majadiliano ya viongozi wa Cyprus yasitishwa kwa muda:UM

Majadiliano ya viongozi wa Cyprus yasitishwa kwa muda:UM

Kiongozi wa Cyprus ya Uturuki Bwana. Mustafa Akıncı, na yule wa Cyprus ya Ugiriki Bwana. Nicos Anastasiades, wamekuwa katika majadiliano mjini Mont Pèlerin tangu tarehe 7 ya mwezi huu chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa katika siku tano zilizopita suala la mipaka na mambo mengine vimejadiliwa na hatu muhimu imepigwa.

Ameongeza kuwa kwa ombi maalumu la kiongozi wa Cyprus ya Ugiriki Anastasiades, imeamuliwa na viongozi hao wawili kuahirisha majadiliano na kuyarejelea tena Jumapili ya Novemba 20 mwaka huu.