Mbinu mpya za kilimo zaokoa wakulima Guatemala
Nchini Guatemala, ukame umekuwa mwiba kwa wakulima, kilimo chao kimekuwa cha mkwamo, wakiwaza kutwa kucha nini cha kufanya ili kunasua maisha yao. Hata hivyo wataalamu wa kilimo wameibuka na mbinu ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabiachi, wakati huu ambapo mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ukitaka wakulima nao wasaidiwe ili kilimo kiwe endelevu. Je ni kitu gani wanafanya? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.