Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi umeanza dhidi ya mlipuko uliojeruhi walinda amani DR Congo:UM

Uchunguzi umeanza dhidi ya mlipuko uliojeruhi walinda amani DR Congo:UM

Uchunguzi dhidi ya mlipuko uliojeruhi walinda amani 32 wa Umoja wa Mataifa kutoka India , raia na kutatili maisha ya binti mmoja raia wa Congo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric walinda amani watano wako katika hali mbaya kutokana na shambulio hilo la Jumanne, na walinda mani wote waliojeruhiwa pamoja na raia wanapatiwa matibabu kwenye kituo cha tiba cha Umoja wa Mataifa Goma. Kuhusu chanzo cha mlipuko huo Stephane amesema

(SAUTI YA STEPHANE)

“Kwa mujibu wa taarifa za awali mlipuko huo ulisababishwa na kifaa kinacholipuka na askari wa kulinda amani pamoja na raia waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu Goma”

Na kuhusu uchunguzi amesema

(SAUTI YA STEPHANE )

“Kikosi cha dharura cha MONUSCO kilipelekwa mara moja kwenye eneo la tukio, na MONUSCO pia imepeleka wachunguzi wakiwemo wataalamu wa vifaa vya mlipuko, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu DRC anatarajiwa kwenda Goma kutathimini hali halisi katika eneo hilo”