Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa zaidi ya milioni watibiwa homa ya ini aina ya C: WHO

Wagonjwa zaidi ya milioni watibiwa homa ya ini aina ya C: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya watu milioni moja katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati wamepata tiba ya homa ya ini aina ya C tangu kuanzishwa kwa tiba mpya miaka miwili iliyopita. Flora Nducha na maelezo kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Katika taarifa yake hii leo , WHO imesema wakati vijiua virusi vifanyavyo kazi moja kwa moja (DAAs) vilipopitishwa kwa ajili ya homa hiyo mwaka 2013, kulikuwa na hofu kuwa gharama kubwa itakuwa kikiwazo cha kuwafikia watu milioni 80 wenye homa ya ini sugu aina ya C.

Shiriak hilo limesemam licha ya mafaniko hayo kwa nchi kama vile Misri, Morocco, Nigeria, Rwanda na Indonesia bado uhitaji ni mkubwa kwa mamilioni ya wagonjwa duniani kote. Kwa mujibu wa WHO, utashi wa kisisa na uwakili wa asasi za kiraia ni miongoni mwa sababu za mafaniko hayo dhidi ya homa ya ini aina ya C ambayo kwa mwaka husababisha vifo vya watu takribani 700,000 ni Dr. Gottfried  Hirnschall, Mkurugenzi wa programu ya HIV na homa ya ini ulimwenguni kwenye WHO.

(Sauti ya Dr. Gottfried )

"Habari njema ni kwamba kile kilichokuwa janga ya kimya kwa muda mrefu, sasa sio, kwa sababu kuna mwamko mpya kote ulimwenguni na nchi zinajitokeza kukabiliana na ugonjwa huu. Na hili si janga tena kwa sabbu tuna dawa ambazo zinaweza kutibu Homa ya ini aina ya C."