Wakimbizi wapya na wa muda mrefu wahitaji msaada

Wakimbizi wapya na wa muda mrefu wahitaji msaada

Watoa misaada ya kibinadamu wanatupia jicho kwa karibu hali ya wakimbizi waliosahaulika na wa muda mrefu, lakini pia wakimbizi wapya katika ngazi ya kimataifa kwa lengo la kushughulikia changamoto zinazowakabili watu hao ambao kutwa wako safarini.

Hayo yamesemwa na mshauri maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu kushughulikia suala la wakimbizi na wahamiaji Karen AbuZayd. Nchi zilipitisha azimio la New York mwezi Septemba ili kulinda na kuokoa maisha ya wakimbizi na wahamiaji.

Wakimbizi na wahamiaji hupoteza maisha kwa maelfu kila mwaka na watu wanaokimbia vita ardhini wanazuilikwa na kufungwa kwa mipaka. Bi AbuZayd anayeondoka katika wadhifa wake anaeleza endapo mkutano na azimio la wakimbizi na wahamiaji limetimiza leo

(SAUTI YA ABUZAYD)

“Tunafikiri limekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa nchi zote 193 wanachama kutia saini utekelezaji wa majukumu, na baadhi ya mambo yaliyoafikiwa ni mazuri kwa wakimbizi na wahamiaji, yataleta mabadiliko katika maisha yao, jinsi gani watakavyoishi, jinsi watakavyopokelewa katika nchi wanakokwenda , na nini kitatokea wakienda katika eneo jipya. Kuna maj   ukumu mengi yanayoambatana na hilo.”