Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitika Afrika Kusini kujitoa ICC

Ban asikitika Afrika Kusini kujitoa ICC

Hatimaye imethibitika kuwa Afrika Kusini imejitoa kwenye mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.

Afrika Kusini iliripotiwa kuwasilisha barua mbele ya Umoja wa Mataifa ikieleza kuwa imefikia hatua hiyo kwa sababu kuwa mwanachama wa ICC kunakinzana na sheria ya nchi hiyo ya haki na kinga za kidiplomasia.

Akizungumzia hatua hiyo mbele ya wanahabari mjini New  York, Marekani, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema..

 (Sauti ya Dujarric)

“Naweza kuthibitisha kuwa barua hiyo imepokelewa na sasa inashughulikiwa na Idara ya masuala ya sheria. Na naweza kusema kuwa Katibu Mkuu amesikitishwa sana na uamuzi wa serikali ya Afrika Kusini.”

Hata hivyo amemnukuu Ban akitambua mchango muhimu wa Afrika Kusini katika kuanzisha mkataba wa Roma na ICC ambapo nchi hiyo iliyokuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kutia saini mkataba huo.

Uamuzi huo wa Afrika Kusini unamaanisha kuwa mwaka mmoja kuanzia sasa nchi hiyo haitakuwa tena mwanachama wa ICC.