Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru ashauri kuwepo kwa mkutano kuhusu ukwepaji kodi.

Mtaalamu huru ashauri kuwepo kwa mkutano kuhusu ukwepaji kodi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atakayechukua nafasi ya Ban Ki-moon anayemaliza muda wake wa uongozi, ameshauriwa kuandaa mkutano wa dunia kuhusu ukwepaji kodi, ulinzi dhidi ya wanaopigia chepuo suala hilo amesema mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa  kuhusu kukuza demokarasia na usawa wa utaraibu wa kimataifa Bwana Alfred de Zayas.

Amesema ikiwa baraza kuu litampitisha António Guterres kuwa Katibu Mkuu ni fursa ya kipekee ya kuendeleza mapamabano dhidi ya ukwepaji kodi na usafirishaji wa fedha haramu wakati huu ambapo dunia inamulika masuala hayo nyeti.

Zayas amesema ana matumaini kuwa ukwepaji kodi na kuanzishwa kwa mamlaka ya Umoja wa Mataifa ya kupinga suala hilo itakuwa kipaumbele cha Guterres na kusisitiza kuwa wakati mabilioni ya dola yakitengwa kwa ajili ya kukabilina na umasikini na mabadiliko ya tabianchi ukwepaji kodi hutowesha mabilioni yadola za umma kila mwaka.

Ameonya kuwa ukwepaji kodi ulionea na unaofanywa kwa siri na taasisi za fedha kama benki, sasa unaripotiwa lakini madhara yake halisi kwa binadamu yanaainishwa taratibu. Ameshauri kuwa suala la kodi liwe ajenda ya baraza kuu, baraza la haki za binadamu hususani katika mkutano kuhusu haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.