Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunasikitishwa na machafuko Myanmar: UM

Tunasikitishwa na machafuko Myanmar: UM

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar, Vijay Nambiar, amesikitishwa na ghasia zilizotekelezwa na watu wasiofahamika dhidi ya walinzi wa mpaka na vikosi vya ulinzi mnamo Oktoba tisa, machafuko yaliyosababisha mapigano na kuuwa raia kadhaa na maafisa usalama.

Kwa mujibu wa tamko lake kwa Katibu Mkuu kuhusu machafuko hayo yaliyofanyika Kaskazini mwa Rakhine nchini Myanmar, Bwana Nambiar ameeleza kuwa amefahamishwa na mamlaka nchini humo kuwa mamlaka za juu zimetaarifiwa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda amani na kuhakikisha machafuko hayaenei.

Mshauri huyo maalum amewataka raia kujizuia kwa kiwango cha juu na kuepuka uchokozi unaoweza kuwafanya wakachukua hatau dhidi ya jamii au makundi ya kidini.

Ametambua jukumu muhimu la vikosi vya usalama nchini Myanmar lakini akavitaka vikosi hivyo kuchukau tahadhari katika siku za usoni ili kuepusha kujeruhi au vifo vya raia wasio nah atria , uharibifu wa mali au ukatili wa aina yoyote ile kwa jamii.