Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aisihi Bangladesh kusitisha adhabu ya kunyongwa dhidi ya Mollah

Pillay aisihi Bangladesh kusitisha adhabu ya kunyongwa dhidi ya Mollah

Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu Navi Pillay amemsihi Waziri Mkuu waBangladeshSheikh Hasina kuagiza kusitishwa kwa adhabu ya kunyongwa dhidi ya mwanaharakati wa kisiasa nchini humo Abdul Quader Mollah aliyepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita katika kesi inayodaiwa kutokidhi viwango vya kimataifa.

Ombi la Bi. Pillay limo katika barua yake kwa Waziri Mkuu Hasina ambapo katika taarifa ya mwezi uliopita, aliisihi serikali hiyo isiendelee na adhabu hiyo iwapo kutaibuka hofu juu ya kuzingatiwa kwa haki kwenye kesi hiyo.

Umoja wa Mataifa unapinga adhabu ya kifo kwa mazingira yoyote ile, hata katika uhalifu wa kupindukia. Wataalamu wawili maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za majaji na mawakili pamoja na mauaji nao pia wametaka hukumu ya kunyongwa hadi kifo dhidi ya Mollah kuondolewa