Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha Haki za Binadamu chahitimisha mazungumzo juu ya utupaji taka, vyombo na madhara yake

Kikao cha Haki za Binadamu chahitimisha mazungumzo juu ya utupaji taka, vyombo na madhara yake

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo limehitimisha mjadala wake ulioleta pamoja kikosi kazi kuhusu matumizi ya mamluki kama njia ya kukiuka haki za binadamu na mtaalamu huru wa umoja wa mataifa kuhusu athari za ukiukwaji wa haki za binadamu zitokanazo na utupaji hovyo taka.

Katika kikao hicho mwenyekiti wa kikosi kazi hicho Patricia Arias amesema sheria dhidi ya ugaidi zinatumika kirahisi na serikali na hatua hiyo inahatarisha ulinzi wa haki za binadamu kwa kuwa husababisha ukiukwaji wa haki hizo.

Bi Arias amesema inakuwa vigumu sana kutekeleza sheria dhidi ya mamluki na badala yake serikali zinatumia sheria dhidi ya ugaidi.

Naye mtaalamu huru Baskut Tuncak,ameonya kuwa karibu asilimia 30 ya vifo vinatokana na sababu za mazingir, akisema kuwa licha ya hivyo bado ni rasilimali chache zinatengwa kushughulia madhara hayo.